Burudani

Majibu ya DNA ya mtoto wa Nay wa Mitego yatoka

Majibu ya kipimo cha DNA ambacho rapper Nay wa Mitego alisema amechukua ili kujiridhisha iwapo mtoto aliyezaa na ex wake Siwema ni wa kwake kweli ama lah, yametoka.

11098721_1560368824232222_1034048252_n
Nay akiwa na mtoto wake Curtis

Kwa mujibu wa Nay ambaye ameachana na mama watoto wake, Siwema hivi karibuni, majibu aliyopata ni ‘mazuri’ na kwamba mtoto ni wake.

“Majibu mazuri, mtoto ni wangu lakini kwa hili lililotokea si la kawaida. Mimi nimeanza life yangu mpya najua nianzie wapi na nitaishia wapi,” amesema Nay.

“Lakini for this time sio muda muafaka wa kuwa na mwanamke, kwa sababu naona nitakuwa naishia sehemu zile zile tena. Pia mama yangu amenishauri kuwa makini kwenye kuchagua aina ya mwanamke.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents