Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Majanga mengine yamkuta Mariah Carey mwaka huu

By  | 

Mariah Carey ni miongoni mwa mastaa waliouanza mwaka 2017 vibaya. Baada ya kuimba vibaya katika show ya kipindi cha Dick Clark’s New Year’s Rockin’ Eve cha ABC na sasa nyota yake ya heshima ya Hollywood Walk of Fame imeharibiwa.

Mtu mmoja asiyejulikana anadaiwa kuchora alama ya kuuliza mwisho wa jina katika nyota hiyo na sasa inasomeka ‘MARIAH CAREY?’.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, maafisa wa jeshi la polisi kutoka mjini Los Angeles hawajachukulia jambo hilo kikawaida kwa kuwa tayari wameanza uchunguzi kwa ajili ya kupatikana mtu huyo aliyefanya kitendo hicho.

Inadaiwa kuwa gharama ya kurekebisha nyota moja huwa ni kiasi cha dola 1,500. Mwezi Oktoba mwaka jana mtu aliyefahamika kwa jina la James Otis aliharibu nyota kama hiyo ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW