Habari

Majambazi wawili wauawa Tanga, walikuwa na bendera yenye maneno ya kiarabu

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na askari wa jeshi la polisi katika misitu ya milima ya Usambara wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

e88a7878

Akizungumzia kutokea kwa tukio hilo mkoani humo, kamishna oparesheni na mafunzo ya jeshi la polisi, Nsato Marijani Nsanzya, amesema tukio hilo limetokea wakati jeshi hilo lilikuwa kwenye oparesheni baada ya kuwatafuta wahalifu baada ya tukio la kuvamiwa kwa chuo cha Sekomu wilayani Lushoto usiku wa kuamkia Oktoba 2 ambapo jeshi hilo liliweza kukamata silaha.

Katika kukamata baadhi ya silaha walizokuwa nazo majambazi hao walikutwa na bendera yenye maandishi ya kiarabu na kamishna huyo aliweza kutoa ufafanuzi juu ya bendera hiyo.

“Sisi hatuamini kwamba bendera hizi na maneno waliyosema yana mahusiano yoyote na dini ya kiislamu,hili ni genge tu ,ni genge la majambazi ni genge la wauaji wanataka kutumia ideology hii kuficha ubaya wao. Sisi sio mashehe lakini tunaijua dini ya kiislam kwasababu miongoni mwetu ni waislamu, hakuna uislam unaoruhusu kuua watu wengine,hasa kuua pale ambapo unaua na kupora na wizi,” alisema Nsato

Aidha kamishna Nsato aliwaonya wahalifu wenye nia ya uovu na jamii akisema, “Uhalifu haulipi na kamwe hautolipa na kwamba mtu asifikirie kwamba anapambana na jeshi la polisi atakuwa anajipoteza. Kwasababu hii ni nchi ya watanzania, ni nchi ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama katika mapambano ya aina hii. Tunaunganisha nguvu vyombo vyote vya ulinzi na usalama hawawezi kupona,” alionya.

Watu waliofariki katika majibizano hayo ni pamoja na Modrick Abdi mwenye umri wa miaka 24 maarufu kama Osama mkazi wa Mbagala na Sultan Abdallah mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Kiembe Samaki Zanzibar.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents