Habari

Maiti Yaibukia Mlangoni Mwa Mtu

Ama kweli Jiji hili la Dar es Salaam linaloongozwa na Bwana Abbas Kandoro lina visa na mikasa, raha na karaha tele! Hebu fikiria mshtuko alioupata mama huyu baada ya kuamka na kukuta maiti na sanda yake imetulia tuli mlangoni mwake!

Ama kweli Jiji hili la Dar es Salaam linaloongozwa na Bwana Abbas Kandoro lina visa na mikasa, raha na karaha tele! Hebu fikiria mshtuko alioupata mama huyu baada ya kuamka na kukuta maiti na sanda yake imetulia tuli mlangoni mwake!

Tukio hilo ambalo wengi wamelifananisha na mauauza ya kishirikina, limetokea leo alfajiri huko Yombo Yombo Makangarawe Jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kwa mhanga wa tukio hilo zinadai kuwa maiti hiyo ilikuwa imesokotwa kwenye kitaamba cheupe na cheusi.

Mauzauza hayo yametokea kwenye nyumba inayomilikiwa na Bi. Rehema Mbisa, mkazi wa Yombo Makangarawe.

Maiti hiyo ya mtoto wa kike asiyefahamika na anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka tisa na 12, ilikutwa na mtoto wa mwenye nyumba hiyo, aitwaye Mary mara tu alipofungua mlango wa nje leo alfajiri.

Akiongea na gazeti hili, mwenye nyumba huyo, amesema mapema leo alfajiri mishale ya kama saa 11:45 hivi, wakiwa wanajiandaa kutoka kuelekea kwenye mizunguko ya kila siku, mwanae huyo wa kike aliyemtaja kwa jina la Mary alitoka lakini alipofika nje ya nyumba yao, akashtuka kukuta kuna kitu kimelazwa mlangoni.

“Alirudi ndani mbio huku akipiga kelele,“ amesema Bi. Rehema.

Amesema walipotoka pamoja, walikuta kitu hicho kikiwa pale pale laliki walishindwa kukitambua, hali iliyowafanya kumuita jirani yao Mzee Mtibi ambaye naye aliwashauri kwenda kuita mjumbe wa eneo hilo.

Amesema mjumbe wa eneo hilo, Bw. Juma Mtauka alipofika, alijaribu kufungua sanda hiyo ili kujua ndani kuna nini.

“Ile kusogeza sanda, akakumbana na vidole vya binadamu. Tuliamua kwenda kutoa taarifa polisi kwa kuwa tukio hilo tuliona si la kawaida,“ akaendelea kusimulia Bi. Rehema.

Amesema alikwenda kituo kidogo cha polisi cha Yombo Makangarawe ambapo askari walitumwa kwenye tukio na yeye akabaki huko kituoni akiandika maelezo.

Ameongeza kuwa polisi hao walipofika eneo hilo walifungua kitu hicho na kuikuta maiti ya mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka tisa na 12. Hata hivyo amesema hawakuweza kuitambua .

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Kandihabi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini akaongeza kuwa anasubiri taarifa zaidi toka kwa vijana wake aliowatuma eneo hilo la tukio

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents