Habari

Maisha baada ya BBA: Annabel afunguka juu ya mpango wa kuungana na Elikem kibiashara baada ya The Chase

Faida za reality show ya Big Brother ‘The Chase’ zimeanza kuonekana (japo kwa mipango) kwa baadhi ya washiriki ambao wameitumia nafasi ya kukutanishwa na washiriki wa nchi mbalimbali na kukuza majina yao kama fursa ya kutengeneza michongo mengine ya kimaisha.

Annabel mbaru
Annabel

Pamoja na kwamba wapo ambao wameendeleza mahusiano ya kimapenzi waliyoyaanzisha kwenye The Chase, akiwemo Koketso wa Afrika Kusini ambaye alifunga safari kumfuata LK4 nchini Uganda siku chache zilizopita.

Annabel Mbaru aliyekuwa mshiriki wa Kenya aliyetoka weekend iliyopita ameonekana kuitumia fursa ya The Chase kimaendeleo zaidi baada ya kuonesha nia ya kuungana na mshiriki wa Ghana Elikem ili kuendeleza fani yao ya fashion baada ya The Chase.

Annabel ambaye ni msomi anayechukua shahada ya uzamili ‘Master’s degree’ na pia ni ‘fashion designer’ amesema akiwa mjengoni yeye na Elikem walizungumza mpango wa kuja kuunganisha nguvu zao katika kukuza brand zao za fashion hapo baadaye, “Elikem has a passion for fashion. We spoke at length about working together after leaving the house”.

AnnabelRisper

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasili Kenya akitokea Afrika Kusini , Annabel pia alisema walipokuwa mjengoni walizungumza pia kuhusiana na kujua kufanya kitu kama ‘The Chase Tour’ ambayo itawawezesha kila mmoja kushiriki katika kile anachokiweza zaidi na kutoa mfano wa Feza na Cleo watakuwa wakiimba na kila mtu atafanya kitu chake. “In fact, we discussed having something like The Chase Tour, where we would have everyone on board doing what they do best; Cleo and Feza with their music, and other stuff like that”.

SOURCE: DSTV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents