Burudani

Mahakama yampa Chris Brown adhabu nyingine

Chris Brown ataendelea kusota na adhabu za jela japo kwa kazi za nje. Kwa mujibu wa TMZ, hitmaker huyo wa Loyal aliyependa kizimbani jana kusikiliza maendeleo ya msala wake, atakuwa busy hadi Januari 2015 kutumikia kazi za jamii.

1023-chris-brown-court-tmz-2

Chris Brown amepewa ‘adhabu’ ya kufanya kazi za kijamii kwa masaa nane kila siku, na kwa mujibu wa ratiba aliyopewa na mahakama anatakiwa afanye kazi hizo kwa siku 4 kila wiki, ikiwa ni siku 1 tu ndani ya wiki kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambazo atakuwa na mambo yake mengine.

Daktari wake alijaribu kupeleka utetezi wake kwa Chris ili kumnusuru na adhabu hiyo hiyo kutokana na matukio kadhaa aliyoyafanya kipindi akiwa chini ya uangalizi wa mahakama juu ya mwenendo wake baada ya kukabiliwa na kesi ya kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents