Michezo

Mahakama yaamuru Liverpool kuuzwa

 


Hatimaye mahakama kuu imeamuru kwamba wamiliki wa klabu ya soka ya Liverpool Ton Hicks na George Gillett kuruhusu mchakato wa timu hiyo kupigwa bei.


Jaji Floyd alitupilia mbali pingamizi la wamiliki hao katika kesi iliosikilizwa jana na hivyo uamuzi huo umeufanya bodi ya wakurungezi wa klabu walioibua wazo la timu kuuzwa kuibukuka kidedea.

Jambo hilo ni ushindi mkubwa kwa mwenyekiti wa Liverpool Martin Broughton ambaye aliweka sawa mipango ya kuipiga bei klabu hiyo ya Anfield.

Baada ya jaji huyo kutoa uamuzi huo wapenzi wa Liverpool walionekana wakifurika katika mji wa Liverpool wakiwa wamevalia jezi za Liverpool na mabango makubwa yakuonyesha kuwa wanataka timu iuzwe.wakisema wanahitaji mabadiliko makubwa Liverpool.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents