Habari

Magazeti mawili  yapewa onyo na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika ziara yake mkoani Singida ametoa onyo kwa magazeti mawili ambayo amesema yamekuwa yakiandika habari za kupotosha wananchi.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo akiwa mkoani Shinyanga.

“Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi, hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi, chini ya utawala wangu hilo halitokuwepo,” alisema Rais Magufuli.

“Kuna Magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu, ikizungumzwa habari hii wao wanageuza, nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia na wasikie, wasiposikia wasisikie. Magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana,” alisisitiza.

Rais Magufuli alitoa onyo hilo bila kuyataja magazeti hayo ni lipi na lipi.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents