Habari

Magari yanayotumia gesi kuanza kuingia nchini Desemba

Kampuni ya Hyundai East Afrika Ltd, imeahidi kuanza kuingiza nchini magari yanayotumia gesi asilia mwishoni mwa mwaka huu.

Na Joseph Mwendapole

 
Kampuni ya Hyundai East Afrika Ltd, imeahidi kuanza kuingiza nchini magari yanayotumia gesi asilia mwishoni mwa mwaka huu.

 

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Mehboob Karmali, aliliambia gazeti hili katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 

Alisema wameamua kuanza kusambaza magari hayo ili kuepusha uharibifu wa mazingira.

 

Aliongeza kuwa wameshazungumza na Korea
Kusini ambao ndio wanaotengeneza magari hayo na wamekubaliana namna ya kufanya biashara hiyo.

 

Alisema gari linalotumia gesi asilia lina gharama ndogo kulinganisha na yanayotumia mafuta ya dizeli na petroli.

 

“Sehemu ambayo utakwenda kwa mafuta ya shilingi laki moja, gesi utatumia ya shilingi 50, 000,“ alisema.

 

Aidha, alisema kwa sasa wanaangalia namna ya kuweka miundombinu kwa ajili ya watu kujaza gesi watakaponunua magari hayo.

 

Alisema nchini Korea magari hayo yameanza kutumika miaka minne iliyopita.

 

Bw. Karmali alisema nchini Brazili nako magari hayo yamekuwa yakitumika kwa wingi na kwamba karibu nchi 38 duniani zinatumia magari hayo.

 

Source: Nipashe

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents