Habari

Mafanikio ni muhimu lakini unahitaji kujitambua namna unavyotaka kufanikiwa

Watu wengi waliofanikiwa duniani wameweza kufanya na kuendelea kuishi kwa kuwa na tabia nzuri. Wanahakikisha kila wanachokifanya kila siku kina makusudi ya kufikia kule wanakotaka wawe.

beautiful customer service operator woman with headset

Tabia ambayo umeanza kuifanya miaka michache iliyopita ndio inayoonyesha wewe leo uko wapi. Unaweza kukubaliana au kutokubaliana. Watu wengi hatuna tabia nzuri na kufanya maisha yetu kubadilika kila siku na sisi wenyewe kukosa furaha. Kama unataka mafanikio makubwa kuna baadhi ya tabia au mambo ya kuzingatia kila siku ili kufikia malengo yako.

Hapa nimeeleza kwa ufupi baadhi ya mambo au tabia zitakazo kufikisha na kukusaidia kupata matokeo mazuri kuelekea mafanikio yako;

1.Elekeza nguvu zako kwenye malengo yako. Unatakiwa kujifunza namna ya kuelekeza nguvu zako kwenye mambo ya msingi na yenye tija kuelekea kwenye malengo yako. Watu wengi tunafanya makosa kwakuwa tunaelekeza nguvu nyingi kwenye vitu visivyo vya msingi. Inakubidi ukae chini na kujiuliza je mambo gani kwako yanatakiwa kupewa kipaumbele kikibwa zaidi kuliko mengine? Je ni mambo gani kwenye biashara yanaweza kuleta faida kubwa na uweke nguvu kubwa huko, usifanye kila kitu katika nguvu sawa.

2. Uwezo wa kupangilia mambo kulingana na Umuhimu wake Fikiria jambo gani ni lamsingi na la maana sana kwa sasa. Chagua jambo hilo halafu elekeza nguvu zako huko. Watu ambao wana matokeo makubwa katika maisha yao na biashara zao huwa hawapotezei fursa wala kupotezea mwelekeo wa kile wanachokifanya.

3. Hufanya miradi na kumaliza majukumu yao  Kama una uwezo wa kuanza kitu na kukifuatilia mpaka uone mwisho wake, huo ndio uwezo wa kufanya tunaouzungumzia. Hapa hatuzungumzii mtu anayebahatisha au kujaribu kufanya mambo. Hebu fikiria ni mambo gani ambayo umewahi kuanza na kuyamaliza? Kama ulianza ukashindwa kumaliza tatizo lilikuwa ni nini?

4. Kuwa na mtizamo chanya katika mambo unayofanya Unapohitaji mafanikio unahitaji mawazo na mtizamo chanya wa kile unachokifanya. Ukikosa kuwa na mtizamo chanya utaishia kufanya kawaida au kutokufanya kabisa.

Watu wengi waliofanikiwa wamepitia vikwazo na kushindwa kwingi. Kama wangeamua kuacha na kutoendelea wasingefika hapa tunapowaona bali waliendelea kutokata tamaa. Hivyo unapokuwa na mtizamo chanya unaweza kufikia viwango vikubwa kwani hutakatishwa tamaa katika mambo ambayo yanashindwa au kuelekea kuShindwa utaendelea kufanya mpaka uone matokeo unayoyahitaji.

Haijalishi maisha yako kwa sasa yako katika mfumo gani bali unaweza kufanya zaidi ya hapo. Kila wakati unapojitahidi kufanya vizuri zaidi, kuwa mtu bora zaidi, kuboresha ujuzi wako na taaluma yako, unapoendelea kuboresha namna unavyowasiliana na watu na vitu vingi unajikuta thamani yako inaongezeka na kuwa nzuri kwa ubora wa hali ya juu. Thamani yako inapoongezeka na mafanikio yako yanaendelea kukua zaidi.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents