Burudani

Madonna aachia nyimbo sita kwa mpigo kama zawadi ya X-mas baada ya album yake kuvuja

Madonna amewapa mashabiki wake zawadi ya sikukuu kwa kuachia nyimbo sita zinazotoka kwenye album yake mpya.

rebel heart

Lakini sio tu kwamba ameamua kwa mapenzi yake kuachia kiasi hicho kikubwa cha nyimbo kwa mara moja, bali ni kufuatia album yake iitwayo “Rebel Heart” kuvuja na kulazimika kufanya hivyo.

“Nilikuwa natarajia kuachia single mpya ‘Living for Love’ kwenye Valentine’s day pamoja na album ingefuatia…” alisema Madonna. “Ningependa mashabiki wangu kusikiliza baadhi ya nyimbo zilizokamilika badala ya vipande vya nyimbo zilizosambaa. Naomba mchukue hizi nyimbo sita kama zawadi ya mapema ya Christmas.”

Nyimbo alizoachia Madonna ni “B*tch I’m Madonna” aliomshirikisha Nicki Minaj, “Living for Love”, “Devil Pray”, “Ghosttown”, “Unapologetic B*tch”, pamoja na “Illuminati”.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents