Burudani

Madj na watangazaji wanatubania sisi wasanii wa Zanzibar – AT

Msanii anayetokea Zanzibar, AT amesema wasanii wengi wa visiwani humo wanafeli sababu madj na watangazaji wa redio wanawabania.

AT-PICHA-3

AT ameiambia Bongo5 kuwa wadau wa muziki inabidi wakumbuke kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

“Naona kuna watangazaji na Madj hawataki kuona wasanii wa Zanzibar wanakuwa wanafanya vizuri, wanaona kama msanii wa Zanzibar akifanya vizuri sifa itaenda Zanzabir na wakati wasanii wote wa bara Zanzibar wanafanya vizuri,” amesema AT.

“Mimi naelewa kwakuwa nimeshafanya research. Wajue wote siye ni Watanzania na waangalie pia maslahi ya taifa maana hii itaenda huko mbeleni italeta matatizo. Nadhani hilo ndio tatizo hasa. Waache hiyo tabia maana ukionana nao na kuongea nao wanakupa ushauri mzuri sana ila lazima tu watambue kuwa shetani hafungwi jela.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents