Habari

Madereva pikipiki Bajaj, teksi watwangana Dar kugombea abiria

KITUO cha daladala cha Mwenge jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa muda kiligeuka kuwa uwanja wa mapambano kati ya madereva teksi na madereva wa pikipiki aina ya Bajaji waliokuwa wakitwangana ngumi kwa kile kinachodaiwa kugombea abiria.

Na Furaha Kijingo

 

KITUO cha daladala cha Mwenge jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa muda kiligeuka kuwa uwanja wa mapambano kati ya madereva teksi na madereva wa pikipiki aina ya Bajaji waliokuwa wakitwangana ngumi kwa kile kinachodaiwa kugombea abiria.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwandishi wa Mwananchi, baadhi ya madereva hao walieleza kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu na awali walilifikisha suala hilo katika kituo cha polisi cha Mabatini kilichopo Kijitonyama na Mkuu wa kituo hicho aliwaahidi kulishughulikia.

 

Akielezea sakata hilo, Katibu wa Umoja wa wa Madereva wa Bajaji, Kuli Swai, alisema chanzo cha ugomvi huo ni kiwango cha bei wanayowatoza abiria kinatofautiana na kile cha teksi kwani wao hutoza bei ndogo kitendo ambacho kinapelekea madereva taksi kukosa abiria.

 

�Sisi abiria mmoja tunamtoza Sh250 kama wakiwa watatu, lakini kama pekee ni Sh700 tofauti na taksi ambayo ni sh 3,000� alisema Swai

 

Hata hivyo Swai aliongeza kuwa wamiliki wa pikipiki hizo wamekuwa wakilipa kodi ya mapato ambayo ni Sh 95,000 kwa mwaka pamoja na kuchangia michango mingineyo ya kijamii mfano ujenzi wa madarasa.

 

Kwa upande wake, Taitas Akolo, dereva taksi alimweleza Mwandishi wa gazeti hili kuwa kuwepo kwa pikipiki hizo kituoni hapo kumepelekea kuua soko la teksi kwani wateja wengi wamekuwa wakikimbilia pikipiki hizo kutokana na kutoza bei nafuu.

 

Hata hivyo, Akolo aliiomba serikali kuzihamisha pikipiki hizo zipelekwe maeneo ambayo hakuna uwezekano wa kupitisha magari ili biashara ya teksi kituoni hapo iweze kuendelea kama kawaida.

 

�Serikali iwahamishe watu hawa wa bajaji iwapeleke maeneo ambayo magari hayawezi kufika huko, kuwepo kwao kwetu ni hali ngumu,� alisema Akolo

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents