Burudani

Madee: Wasanii tunarekodi nyimbo mfululizo ndio maana hazihit

Muimbaji wa Tip Top Connection, Madee amedai kuwa nyimbo nyingi za wasanii zinashindwa kufanya vizuri kutokana na wasanii kuingia kurekodi nyimbo kila siku.

Madee2

Madee ameiambia Bongo5 kuwa ili msanii awe mtunzi mzuri anatakiwa kukaa walau miezi sita kabla ya kuandaa wimbo mwingine.

“Wasanii wanatakiwa kujipa muda tu, unajua wasanii wanakosea hili kwa sababu kila siku wanataka wakarekodi kwa sababu yeye tu ni msanii mkubwa studio anaweza kwenda muda wowote na kufanya chochote,” amesema Madee. “Unakuta studio time halipi au labda studio yake kwahiyo anataka kila siku awe anarekodi. Hiyo inakuwa mbaya kwa sababu unakuwa hauandiki kitu kizuri na wala huwezi kupata more ideas kila siku ukiwa unarekodi.”

“Mimi mwenyewe najipaga time nikisharekodi wimbo mmoja sirekodi kwanza mpaka baada ya miezi sita, so miezi sita yote ambayo nakuwa kimya najaribu kuangalia soko linavyoenda, maneno gani yanatakiwa kwa sasa ndo kitu ambacho nakizingatia.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents