Burudani

Madee atoka nje kwa dhamana baada ya kuhusishwa na tukio la utekaji

Muimbaji wa Tip Top Connection, Madee hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuwekwa ndani katika kituo cha polisi cha Kigamboni kutokana na madai ya kuhusishwa na tukio la utekaji.

Hamad Ali aka Madee

Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo, Babu Tale, mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown aliripoti kupitia ‘You Heard’ ya XXL kuwa Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’

Babu Tale alisema: Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora,kwahiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki halafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma. Pikipiki ilivyodondoka yule aliyekua nyuma kwenye pikipiki ambaye ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliyekuya anaendesha hiyo pikipiki.

“Wakamchukua na kwenda nae maskani TipTop,” ameeleza Tale. Mama yake akaja akasema ‘msipeleke polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu. Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake, saa nne asubuhi yule mama akaja na polisi badala ya kuja na mwizi, mwenzake akaja na polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop. Walimchukua huyo mhalifu kwenye Land Rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa.”

“Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka hospitali. Nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa polisi akaripoti, kufika kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka hospitali akawaambia ‘huyu ni mwizi ameiba’ Ikabidi dogo aingizwe ndani jana akalala pale olisi Magomeni.

“Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufuata mhalifui wake na kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni. Saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia meseji anasema Madee analalamika mbona humfatilii, nikauliza ‘kuna nini tena’ akasema wamemuingiza ndani. Nikapiga simu polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu. Nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana, ni hilo, yataisha kama yalivyoanza’

Bongo5 leo imemtafuta Madee aliyesema yupo vizuri ila kwa sasa hawezi kuongelea kitu chochote kuhusu tukio hilo.

Source:Millardayo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents