Burudani

Madee atoa sababu ya kubadili ratiba ya ujio mpya wa Dogo Janja

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee ambaye aliwaahidi mashabiki wa kundi hilo kuwa Dogo Janja ataachia wimbo hivi karibuni, amedai ameahirisha mpango huo kutokana na kuingiliana kwa ratiba nyingine.

Madee na Chege akiwa kwenye pozi

Akizungumza na Bongo5 leo, Madee amesema imelazimika Dogo Janja asubiri kwakuwa kuna wimbo aliofanya akiwa na Chege na Temba Afrika Kusini unayohitajika kutoka mapema zaidi.

“Kuna mabadiliko kidogo ambayo yameingiliana,” amesema rapper huyo. “Kuhusu Dogo janja bado kidogo yupo ningependa kuzungumzia ratiba inayofuata ya Madee, kwa sababu kuna project ambayo tulienda kufanya South Africa kule inatakiwa itoke mapema Januari kwahiyo hicho ndo kitu ambacho kinaangaliwa sana. Then Dogo Janja atakuja pamoja na Raymond. Kwahiy mwakani itatangulia kwanza nyimbo ya Madee na baada ya hapo ndo Dogo Janja atakuja.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents