Burudani

Madee amzungumzia Raymond kwa mara ya kwanza tangu ajiunge WCB

Madee afunguka kuhusu Raymond kwa mara ya kwanza tangu aachie wimbo wake wa ‘Kwetu’ chini ya WCB.

12530931_1134578353259492_799030960_n

Madee ambaye ndiye alimuunganisha Raymond kwenye kundi la Tip Top Connection kabla ya kujiunga na lebo ya WCB.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Madee amesema, ‘ninachokiona nilikitarajia kwamba Raymond atakuwa mtu fulani’.

“Raymond yuko vizuri anafanya vizuri ni mtu ambaye nimekaa naye najua uwezo wake, ninachokiona nilikitarajia kwamba Raymond atakuwa mtu fulani, Raymond ana kila kitu ambacho msanii anatakiwa awe nacho, mara nyingi huwa naenda nae studio,” aliongezea Madee.

Madee kwa sasa ameachia nyimbo yake ‘Migulu Pande’ ambayo imeanza kufanya vizuri kwenye media mbalimbali japo haina muda mrefu tangu aitoe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents