Habari

Madee amchana Lundenga kwenye ngoma mpya , ‘hao Ma-miss wazee kama vipi mwaka kesho namleta bibi yangu agombee’

Wimbo mpya wa Madee ‘Vuvula’ haukuishia kumchana Chidi Benz peke yake(Ingia hapa) , upo mstari mwingine ambao unamlenga Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga

Madee2

Mstari huo unasema: “Hey Anko Lunde, hao Mamiss wazee kama vipi mwaka kesho namleta bibi yangu agombee.”

“Kuna tatizo lilitokea lilipita kuhusu mamiss nini, so nimejaribu kumwelewesha tu ambaye ni Vuvula ajaribu kuwa makini baadae akiwa anasajili mamiss wake”. Alisema Madee alipokuwa akielezea maana ya wimbo wake.

Madee aliwahi kusema kupitia moja ya vituo vya radio kuwa maana ya Vuvula ni “mtu mshamba ambaye hajielewi.”

So Madee, unamaanisha Anko Lunde ni Vuvula? Lol!

Ingia hapa kumskiliza Madee mwenyewe akielezea.

Chanzo: EATV

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents