Burudani

Madam Rita asema ukiritimba umewakwamisha wasanii kupiga hatua

Jaji wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS), Madam Rita amesema ukiritimba uliopo kwenye mazingira yanayowazunguka wasanii wa muziki unakwamisha maendeleo yao.

Jaji mkuu wa shindano la BSS 2015,  Madam Rita Paulsen

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa hoteli ya Regency, Madam alisema wasanii wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na kushindwa kujikwamua wenyewe.

“Kuna vitu hatuwezi kuvicontrol, huwezi kucontrol media na ukiritimba uliopo kwenye media na vitu kama hivyo. Mimi BSS inatoa platform ya kuonekana, wapo wengi wanafanya vizuri, walio tayari kubebeka tuliwabeba, ndio maana mwaka huu tukaweka kampuni kama Tip Top iweze kusimamia,” alisema Rita.

“Hii ni moja ya changamoto lakini ipo siku itaisha, kila bendi ya Tanzania inamshiriki wa BSS, Msuya alikuwa anaendesha boda boda lakini sasa hivi ameajiri vijana 29, anaingiza laki 9 kwa wiki. Inategema kufanya vizuri ina maana gani kwako, kusikika kwenye redio sio kufanya vizuri, wanalipa watu ili wasikike.” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents