Michezo

Macheda: Nilifanya makosa kuondoka United kwa mkopo

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United, Federico Macheda amesema alifanya makosa alipokubali kutolewa kwa mkopo.

federico-macheda-manchester-united

Macheda ni miongoni wa wachezaji waliokuwa wanaonekana kufanya vizuri na kutabiriwa kuja kufanya mambo makubwa baadae kwenye timu yake ya United na timu yake ya taifa ya Italia. Amesema sababu kubwa ambayo imechangia kwa yeye kushuka kwa career yake ni kutolewa sana kwa mkopo na timu yake hiyo ya zamani.

“Sir Alex Ferguson aliniambia siyo mbaya nikienda kucheza kwa mkopo itanisaidia kuwa fiti kwa season zinazofuata” alisema Macheda.

Aliongeza pia, “Sijui kwanini nilienda Italia. Lilikuwa ni kosa kubwa sana kwa kipaji change. Ningebaki tu Uingereza.”

Kwa sasa mchezaji huyo anaichezea timu ya Cardiff City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents