Burudani

Mabeste: Nilisimama kufanya muziki ili kuwa karibu na mwanangu

Rapper Mabeste amedai kuwa ilimbidi asimame kufanya muziki kwa mwaka mmoja na zaidi ili kutenga muda wa kutosha wa kukaa nyumbani na mwanae wa kiume, Kendrick.

Mabeste

Mabeste amesema kutenga muda huo ilikuwa ni muhimu kwake ili kumpa nafasi mwanae kumfahamu zaidi baba yake na pia kutumia muda huo kufanya shughuli zingine za kumuingizia kipato tofauti na muziki ambao anadai kwa miaka 10 alioutumikia haujampa kipato cha kueleweka.

“Nimekaa na mtoto wangu niliacha kazi kabisa. Nilikuwa nafanya kazi za kawaida tu ili mtoto wangu aweza kuishi maisha ambayo ndani yake niweze kulipa kodi ya nyumba, mtoto aweze kupata pampers. Ili muziki nilistop kiukweli,” Mabeste ameiambia Bongo5.

“Hata studio nilikuwa siendi kabisa. Nilitaka kufurahia kidogo na mwanangu. Nilifanya muziki kwa zaidi ya miaka 10 na sijapata cha maana kwahiyo nikitumia kama mwaka mmoja na mwanangu ni bora zaidi. Huu muda wa mwanangu ukipita kukaa naye haiwezi kujirudia tena.”

Mabeste amesema kwa sasa amerejea tena kwenye muziki na anatarajia kutoa wimbo mpya aliomshirikisha Jux pamoja na video ya wimbo wake ‘Nishauri’ aliomshirikisha Peter Msechu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents