Burudani

Mabeste kuzindua documentary ya maisha yake Jumapili hii

Ni mengi yamejitokeza katika maisha binafsi na ya muziki ya rapper Mabeste, ukiachilia mbali ishu yake na B Hitz lakini pia amefanikiwa kuwa baba, yote hayo na mengine yatapatikana katika documentary yake.

Mabeste

Mabeste amesema documentary ya maisha yake itazinduliwa Jumapili hii (April 27) pale Club Billicanaz.

“kuna vitu vingi sana ndani ya hiyo documentary, historia yangu ya maisha, wapi nimetoka wapi naelekea” Amesema Mabestee.

Rapper huyo ameongeza kuwa atakuwa akizindua kwa episode hivyo baada ya wiki hii ataendelea katika club zingine kwa wiki zijazo kuzindua episode zitakazofuata.

“Ni mwendelezo sababu ina mwendelezo mrefu sana…kwasababu si unajua documentary ni maisha kwa hiyo bado tunaendelea kushoot kila siku”, alisema Mabeste kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Uzinduzi huo utasindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo M-Rap, Queen Darleen, Suma Mnazareti, Stamina, Country Boy na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents