Tragedy

Mabaki ya viungo vya miili ya binadamu yabainika yalikotoka

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio la kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

140722135451_tanzania_polisi_512x288_michuziblog

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova

Kamanda Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.

10556531_975957895751962_2369365397034521443_n
Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es Salaam

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju. Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.

Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.

Source: BBC picha, hisani ya Michuzi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents