Habari

M-Net waibadilisha Africa Magic Swahili kuwa Maisha Magic Swahili

Kuanzia Jumatano, September 24
kampuni ya M-Net itaibadilisha channel ya Africa Magic Swahili inayoonekana kupitia DStv na GOtv kuwa na jina jipya, Maisha Magic Swahili.

image

Kubadilika kwa jina hilo kunaendana na mabadiliko yaliyoonesha kuzalishwa kwa brand ya Maisha Magic itakayojikita katika kuonesha vipindi vya Afrika Mashariki ama vinavyopendwa na wananchi wake.

Ikifuata baada ya kuzinduliwa kwa channel yenye muelekeo wa burudani Maisha
Magic (DStv channel 161) mapema mwezi huu, Maisha Magic Swahili ni hatua mpya kutoka M-Net kutengeneza channel yenye mambo yanayowahusu wapenzi wa burudani wa Afrika Mashariki.

Akizungumzia kubadilishwa kwa jina hilo, Mkurugenzi wa M-Net wa Afrika Mashariki,
Michael Ndetei alidai kuwa ana matumaini makubwa kuhusiana na mustakabali wa vipindi vya Kiswahili, kama lugha kongwe duniani inayotumika kwa kiasi kikubwa.

“Africa Magic Swahili ilianzishwa mwaka 2011 kutangaza utamaduni wa Kiswahili na kutimiza mahitaji ya jukwaa hilo. Na sasa miaka mitatu baadaye, wakati jina linaweza kuwa linabadilika, dhumuni la kusherehekea vipindi vya Kiswahili bado linaendelea kuwa kuu katika
Maisha Magic Swahili,” alisema.

Kuanzia Octobert 5 channel hiyo itaanza kuonesha filamu za mastaa mbalimbali wa Tanzania ikiwemo ‘Nguvu ya Imani’ ya
Simon Mwapangata aka Rado na Khadija Mohammed pamoja na
Waves of sorrow ya Khadija Mohammed, Rose Ndauka na Vincent Kigosi itakayooneshwa October 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents