Burudani

M 2The P aeleza kilichotokea siku Ngwea anafariki, adai anahisi kuna mkono wa mtu

Msanii wa muziki M 2The P ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa msanii Albert Mangwea, amesema hadi leo anahisi kuna mtu aliyehusika na kifo cha Ngwea, na kumfanya ashindwe kuamini ni ajali ya kawaida.
M2 THE P akiwasha mshumaa kwenye kaburi la rafiki yake Mangwea.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, M2The P amesema kitendo cha kuibiwa vitu vyao vyote ndio kilichompa wasi wasi.

“Unajua ile siku tuli-party sana,” alisema M2 The P. “ Tumepiga bata lakini kilichonishtua, ni sawa tukio lilikuwa kama ilivyoonekana ila kilichonishangaza ni baada ya kurudi ghetto tukakuta vitu vyote vimeibiwa, kitu kilichonishtua, ina maana ilikuwa ni kama walitu-target kabisa,”

Pia msanii huyo ambaye naye siku ya tuko hakuwa katika hali nzuri baada ya kupoteza fahamu, amesema kulingana na hali hiyo, anaunga mkono kauli ya mama mzazi wa Ngwea Bi. Denisia Constantino, kwamba huenda kuna watu walishiriki kusababisha kifo cha Ngwea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents