Burudani

Lupita Nyong’o awa chakula cha ma-paparazzi wa Marekani, ajifungia ndani kukwepa usumbufu

Unapokubalika Hollywood na kuwa chakula cha vyombo vya habari vya nje kila kukicha ni dhahiri kuwa tayari unakuwa umeingia katika menu ya mapaparazi. Muigizaji Lupita Nyong’o ameweza kulifanikisha hilo kupitia mafanikio ya movie ya ’12 Years A Slave,’ kiasi cha kuanza kukimbiliwa na kufuatwa na ma-paparazzi kila anapoenda, wakihitaji kupata picha na chochote cha kwenda kuandika.

LUPITA

Star huyo mpya wa filamu kutoka Kenya amesema hajazoea maisha ya umaarufu na hakutegemea kama kazi aliyoichagua ya uigizaji ingekuja kumfanya awe mkubwa kiasi hicho duniani siku moja.

“Nimekuwa nikijifungia ndani, nimekuwa sitoki sana, sijazoea kufahamika kiasi hiki” Lupita aliliambia jarida la New York.

Lupita new york

Lupita ameelezea uzoefu alioupata wa kukimbiliwa na ma-paparazzi ambao kwa nchi za wenzetu huwafuatilia sana watu maarufu kila waendapo kwaajili ya kuwapiga picha na kupata chochote cha kuandika, mambo ambayo tumezoea kuyaona kwa mastaa kama kina Kanye West, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna na wengine.

“Sijui walikuwa wakimsubiri nani, lakini ni dhahiri walinikimbilia , kitu ambacho kinaanza kuwa kero, sikutarajia kitu kama hicho” . Alisema Lupita

Lupita n Pharrel
Lupita na Pharrell

Jumatatu ya wiki hii Lupita alihudhuria luncheon ya nominees wa tuzo za Oscar, na safari hii alikutana na producer na hit maker wa ‘Happy’ Pharrell Williams na wakapiga picha ya pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents