Michezo

Luis Enrique: Jambo gumu zaidi katika soka ni kufunga magoli

By  | 

Kocha Luis Enrique anaamini timu yake ya Barcelona ilifanya jitihada zote kuifunga Villarreal katika mchezo ambao walitoka sare ya 1-1 mechi ya La Liga Jumapili.

Barca walisawazisha goli dakika ya 90 lililofungwa na Lionel Messi na kupata pointi moja katika uwanja wa Estadio de la Ceramica, baada ya Nocola Sansone kufunga goli la mapema katika mechi hiyo.

Luis Enrique, ambaye kikosi chake kilifungwa 2-1 na Athletic Bilbao katika mechi yao ya kwanza ya mwaka 2017, aliumia sana kukosa pointi tatu.

“Timu ilistahili zaidi, tulistahili ushindi, lakini mpira wa miguu hauna haki mara zote,” alisema.

“Villarreal ni timu inayojaribu kucheza, wana wachezaji wenye ubora mkubwa. Wanaujua vema mfumo wao wa uchezaji, wakiwa na mpira na wakiwa wameukosa.

“Tulijua kwamba tungekutana na mechi ngumu dhidi ya Villarreal, lakini tulistahili kushinda. Sina la ziada la kusema kwa wachezaji wangu, tumecheza vizuri.

“Hisia zile nilizokuwa nazo Bilbao, tumecheza zaidi ya pale. Tumetengeneza nafasi nyingi dhidi ya timu ambayo imeruhusu magoli machache zaidi kwenye La Liga, ingawa hatukuwa na usahihi wa kutosha kama ilivyo kawaida yetu kwenye umaliziaji.”

Barca ambayo kwasasa inayoshika nafasi ya tatu sasa ipo nyuma ya Real Madrid kwa pointi tano, na timu hiyo ya Zidane bado ina mchezo mkononi.

“Bado kuna mechi tele za ligi za kucheza, kwa hakika tutakuwa tunazipigania,” aliongeza Luis Enrique. “Hatuna budi kuendelea kujiimarisha, ikibidi kwa nguvu zaidi ya hapa.

“Jambo gumu zaidi katika soka ni kufunga magoli.”

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments