Burudani

Lugha haijawahi kuwa kikwazo cha kufanya kazi na wasanii wa Tanzania – Justin Campos (Audio)

Muongozaji wa video wa Afrika Kusini, Justin Campos amesema lugha haijawahi kuwa kikwazo katika kufanya video za wasanii wa Tanzania.

12783221_848110622002322_1037272663_n

Muongozaji huyo ameongoza video za wasanii kibao wa Bongo wakiwemo Vanessa Mdee, Joh Makini, G-Nako, Ommy Dimpoz na Nedy Music, Shaa, Ben Pol na wengine.

“Sijui Kiswahili, sio zaidi ya kama mtalii wa kawaida lakini haijawahi kuwa kikwazo kufanya kazi na wasanii wanaozungumza Kiswahili kwasababu kila mmoja anazungumza Kiingereza,” Campos alikiambia kipindi cha The Premier cha Kings FM ya Njombe.

“Na siku zote wimbo hufafanuliwa kwetu, sio tatizo kabisa, sijawahi kuwa na issue. Nimefanya na wasanii kwenye kila nchi ya Afrika haijawahi kuwa tatizo. Nadhani Kiingereza ni lugha ya dunia na siku zote huwa tunafanya kazi vizuri,” aliongeza.

Amesema bado haijatokea fursa ya kuja kufanya video Tanzania kwakuwa mahitaji ya video nyingi wanazozitaka wasanii Bongo Flava yapo Afrika Kusini.

Kwenye mahojiano hayo Campos ambaye hufanya kazi na mke wake Candice, alisema hakusomea kazi hiyo zaidi ya kujifunza mwenyewe kwa kusoma mtandaoni na kujifunza kwa waongozaji wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents