Michezo

Louis van Gaal atangaza kustaafu kazi ya ukocha

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal ametangaza rasmi kustaafu kufundisha mchezo huo.

Van Gaal ambaye pia aliwahi kuzikundisha timu kubwa za Ulaya kama Ajax, Barcelona na Bayern Munich amesema kuwa sababu ya kuachana na kazi hiyo ni kutokana na sababu za kifamilia huku akiongeza kuwa tayari amekataa ofa ya £44m kutoka kwa timu ambayo alihitajika aifundishe kwa misimu mitatu.

“I could go there, but I’m still here. So much has happened in my family. I thought maybe I would stop, then I thought it would be a sabbatical, but now I do not think I will return to coaching,” ameliambia gazeti la De Telegraph.

Kocha huyo amekuwa nje ya uwanja tangu alipofukuzwa kuifundisha Man United msimu ulioisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents