Michezo

Liverpool yachapwa Europa League, Shakhtar Donetsk na Sevilla zatoka 2-2

Mechi za nusu fainali za Uefa Europa League zimechezwa jana, mabingwa watetezi Sevilla wakicheza ugenini na Shakhtar Donetsk.
Matokeo ya mchezo huo ni kwamba Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 2-2 ndani ya dakika 90 za mchezo.

article-3564334-33A1CBEE00000578-869_964x386

Sevilla ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 6 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Mchin Perez, na Shakhtar Donetsk kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa Maros Romeo na Stepanenko kuongeza bao la pili dakika ya 35 kipindi cha kwanza.

33A18D1100000578-3564538-image-a-30_1461879790347

Baadaye kelvin Gameiro akaisawazishia Shakhtar Donetsk ikasawazisha bao hilo dakika ya 82 kwa njia ya penati .
Katika mchezo mwingine Klabu ya England Liverpool ikicheza Ugenini huko Uhispania imeambulia kichapo cha bao 1-0 mikononi mwa Villarreal kwa bao la Adrian Lopez la dakika ya 90 ya mchezo.

Timu zote nne zitarudiana tena tarehe Alhamisi wiki ijayo, ikiwa ni mechi za pili hatua ya nusu fainali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents