Michezo

Liverpool waingia nusu fainali ya Capital one

Timu ya Liverpool imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la ligi maarufu kama Capital one .

article-3343438-2F00819500000578-709_964x387

Liverpool ilipata ushindi kwa kuichapa timu ya Southampton kichapo cha mabao 6-1.

Southampton walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Sadio Mane.

2F0048BD00000578-3343438-image-m-63_1449091396265

Liverpool wakakomboa bao hilo kupitia mshambuliaji wao Daniel Sturridge katika dakika ya 29 , Sturridge, tena akaongeza bao la pili.

Mshambuliaji Divock Origi akaongeza mabao mengine matatu katika dakika ya 45, 68, 86, huku Jordan Ibe nae akifunga bao moja, na kukamilisha idadi ya mabao 6.

Michezo ya nusu fainali ya kwanza itafanyika January 5 na 6 na michezo ya marudio ikifanyika 25 na 26 ambapo Liverpool watachuana na Stoke City katika mchezo wa nusu fainali huku Manchester City wao wakikabiliana na Everton.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents