Habari

Lisa Jensen aelekea nchini China kwenye Miss World 2012

Miss Tanzania 2012 Lisa Jensen hatimaye jana amekwea pipa kuelekea nchini China kwaajili ya kuiwakilisha Tanzania kwenye kinyang’anyiro cha Miss World 2012. Tofauti na ilivyozoeleka, Lisa aliteuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya ratiba ya mashindano hayo ya dunia kubadilika na hivyo kuathiri upatikanaji wa kawaida wa Miss Tanzania.
Miss World 2012 ni ya 62 kufanyika na inatarajiwa kufanyika August 18, 2012 kwenye uwanja wa Dongsheng Fitness Center, Ordos, Inner Mongolia, China.
Miss World 2011 Ivian Sarcos wa Venezuela atamvisha taji mrembo wa mwaka huu. Washiriki wote watapata fursa ya kutembelea miji mikubwa ya China ikiwemo Hong Kong, Sanya na Shanghai.
Ifuatayo ni ratiba ya Miss World 2012:
Leo July 18: Washiriki wanawasili mjini Ordos (Crowne Plaza)
July 19-23: Mafunzo wa washiriki, usaili, filming na rehearsals
July 24: Ordos Welcome and Miss World 2012 Opening Ceremony
July 25: Ordos – Hong Kong (ndege ya mchana )
July 26-28: Ziara ya Hong Kong, kujitambulisha kwa washiriki na presentation itakayotolewa na idara ya utalii ya Inner Mongolia.
July 28: Hong Kong – Sanya (ndege ya asubuhi)
July 28-30: Sanya city tour, beachwear filming
July 31-Aug 2: Ziara ya Shanghai, Miss World Charity Dinner (washiriki watakaa Peace Hotel)
Aug 2: Safari kurejea Ordos (Seven Star Lake Resort)
Aug 3: Beachwear filming (The Dunes)
Aug 4: Miss World Beach Beauty Final (Seven Star Lake Resort)
Aug 6: Miss World Sportswomen Final (Miss World library donation)
Aug 7-9: Return to Crowne Plaza, rehearsals for main show
Aug 10: Miss World Talent Final, Ordos Charity Dinner
Aug 11: Top Model show rehearsal
Aug 12: Miss World Top Model Final
Aug 13-17: Miss World Final rehearsals (stadium)
Aug 18: 62nd MISS WORLD FINAL 2012
Aug 19: Contestants depart Ordos

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents