Burudani

Linex na Empty Soulz kumtoa msanii mwenye ulemavu wa viungo

Linex Sunday Mjeda akishirikiana kampuni ya Empty Soulz wameandaa mpango maalum wa kumsaidia mlemavu wa viungo aitwae ‘AZ’

10895477_1405156923112795_1511814733_n
Mlemavu wa viungo aitwae AZ akiwa na Linex kwa nyuma

Linex ameiambia Bongo5 kuwa wamesitisha kuachia wimbo wake mapema kutokana na kuaanda show maalum itakayosaidia kuchangisha pesa za kumsaidia.

“Ambacho tumekiona tukisema tuitoe tu ipigwe redioni au kwenye TV kuna vitu atakosa, sasa tunacho plan kuna kampuni pia imejitokea kumsaidia ‘Emptysoulz Production’ pamoja na Seductive Records ambao walijitolea kumsaidia audio na video. Kitu ambacho tunaplan sasa hivi iandaliwe show fulani tuongee na baadhi ya wasanii wa muziki wa Tanzania ili tuandae show, jamaa ataweza kupata pesa ya kujikimu kwa sababu sasa hivi anaishi maisha magumu sana,” alisema Linex.

Linex

Akizungumzia sababu iliyomsukuma kumsaidia mlemavu huyo, Linex alisema:

“Mama wa huyo kijana anampambania mwanae kwa sababu mume wake alimkataa baada ya jamaa kuwa mlemavu, ndo maana hata jana kwenye line zake kuna vitu ameongea vinagusa sana. Kuna kauli moja alimwambia mama yake ni bora angefariki utotoni mama yake angeweza kupata watoto wengine ambao wangekuwa faraja kwake na msaada kwake kuliko yeye ambae amekuwa mzigo kwake. Huyu mama hana mtoto mwingine na mama alisema hatakuja kupata mtoto mwingine atabakia na huyo huyo mwanae ndiy maana jamaa kwenye wimbo amefikia point anajaribu kumshawishi mama yake kuwa hata na watoto wengine lakini mama yake anapinga kuwa na watoto wengine, kwahiyo jamaa ana story nyingi sana,” aliongeza Linex.

“Jamaa hajawahi kwenda shule na anajua kusoma na kuandika, amejifunza kupitia kanga za mama yake, anaweza kuandika stori, wimbo ameandika mwenyewe, pia jamaa alikuwa hawezi kuongea kutokana na hapati muda wa kukaa na watu na kuzungumza nao. Muda mwingi alikuwa akizungumza na mama yake na mama yake ndo kama hivyo anaamka asubuhi kwenda kutafuta maisha. Kwahiyo maisha ni full mitihani. Sisi baada ya kuona hawezi kuongea tukaanza kumchanganya na vijiwe vya watu ili aweze hata kubishanabishana na kujijengea uwezo wa kuzungumza. Mpaka sasa hivi yupo vizuri ndo maana hata unaona amefanya wimbo na mimi,” alisema Linex.

Linex amewataka pia watu na wadau mbalimbali kushirikiana kwa pamoja kuwasaidia walemavu mbalimbali wanaopatikana kwenye mazingira wanayoishi.

“Najua kuna walemavu wengi wenye talent kwenye jamii, mimi nimefanya hivi kuionyesha jamii kwamba sio kila mlemavu anaweza kuishi kwa kusaidiwa tu na watu kwa kupewa msaada. Kuna walemavu mwenye uwezo wakiwezeshwa, ukimsaidia mlemavu Mungu na wewe atakupa thawabu kwa kile ulichokifanya. Kwahiyo kwenye hilo tamasha ambalo tunaandaa tunaweza kuzungumza mengi ila niwashukuru Solomoni Lamba , Mr T Touch na wengine kwa sababu sio kila mmoja ana moyo wa kusaidia.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents