Burudani

Linex azungumzia collabo na Diamond na ukubwa wa ‘Wema kwa Ubaya’

Msanii kutoka Kigoma, anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Wema Kwa Ubaya’, Linex aka Mjeda amesema wimbo huo ni mkubwa kutokana na ujumbe ulioubeba.

Linex-na-Zitto

Linex amesema hana desturi ya kusikiliza nyimbo zake, lakini kutokana na ujumbe wa ‘Wema kwa Ubaya’ amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara.

“Unajua wimbo wangu wa sasa ‘Wema Kwa Ubaya’ umefanya vizuri haraka nahisi kutokana na muziki ambao nimefanya una ujumbe kwa jamii,” amesema Linex. “Unajua sasa hivi watu wengi wanaimba mapenzi. Wimbo upo tofauti sana, maana sometimes hata mie mwenyewe huwa huu wimbo unanichukua muda mwingi sana, hasa pale ninapousikiliza. Unajua huwa sina taratibu ya kusikiliza ngoma zangu, lakini hii nimekuwa nikisikiliza sana.”

“Huu wimbo nilirekodi miaka mitatu iliyopita. Kwahiyo huu ulikuwa ni muda wake wa kutoka. Lakini huu wimbo, baadhi ya maneno alinipa mheshimiwa Zitto Kabwe. Pia idea ya huu wimbo ilitoka kwenye wimbo wa Aifora, kuna mstari unasema ‘siwezi kukuvua wema na kukulipa mabaya’. Mheshimiwa Zitto akanimbia ‘unajua hilo neno unaweza kupata wimbo ambao utajitegemea’ akaniambia ‘chukua maneno ya Wema badala ya Mabaya, weka kwa ubaya ndo ikawa “Wema Kwa Ubaya”.

Linex amedai kuwa kwa sasa anaandika filamu yenye jina la ‘Wema kwa Ubaya’ na wimbo utakaofuata ni ule aliomshirikisha Diamond.

“Sasa hivi naandika movie ya ‘Wema kwa Ubaya’ ambayo nitawapa watu wengine wafanye. Pia kuna ngoma itakuja baada ya hii ‘Wema kwa Ubaya’ nimefanya na Diamond inaitwa ‘Salima, kwahiyo sasa hivi mashabiki wangu wategemee ngoma baada ya ngoma hakuna kulala.

Linex alizungumzia pia uhusiano na msichana wa kizungu ambaye inasemekana waliachana. “Unajua hatukuachana, sema tulikuwa kidogo kuna vitu tumetofautiana lakini sasa hivi tupo sawa na alikuwa Dar hivi juzi, lakini ameondoka tena.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents