Burudani
Linex adai mademu wa kibongo ‘longolongo’ ndio maana hawadumu kwenye ndoa
Linex amesema anawakubali zaidi mademu wakizungu kutokana na kuwa wakweli katika mahusiano huku akidai mademu wengi wa bongo waongo waongo.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kutoka kimapenzi na demu wakizungu na baadae kuachana , amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii kuwa, mademu wa kibongo longolongo nyingi ndio maana wanaume wengi wanashindwa kudumu nao kwenye ndoa.
“Tofauti ya mapenzi ya kibongo bongo na wazungu iko kwenye uwazi au ukweli. Wenzetu wako ‘real’. Wabongo longo longo nyingi, kudanganyana sana ndio maana watu wanakaa wiki mbili wanaachana. Siri ya mahusiano ni trust.,” alisema Linex