Burudani

Linah na David Banner warekodi wimbo pamoja

Rapper na producer wa muziki kutoka Marekani, David Banner hivi karibuni aliingia studio na producers kutoka Tanzania Lamar, Nahreel, P-Funk Majani pamoja na Ematheboy na kutengeneza beat ambayo baadae David Banner na Linah waliingiza sauti.

4K0A4274 (1024x683)

Akizungumza na Bongo5 leo, mmoja kati ya producer hao, Lamar, amesema waliingia studio na producer huyo ili kukuza uwezo na kubadilishana maarifa.

“Sisi tulikutana tu, tukawa tunatengeneza beats, tumeanza kutengeneza beats tumekata samples pale tukawa tunashauriana tufanye vipi , halafu akaingiza sauti David Banner kama chance tu na Linah akaingiza chorus ikawa bado kuingiza verse, yaani tulikuwa tunafanya kitu kwa pamoja tunatengeneza beats kwa pamoja, project ambayo amefanya Linah na David Banner itaendelea tutafinalize. Kuhusu mambo mengine tulizungumzia kwenye work shop iliyopita kuhusu industry ya muziki jinsi ya kufanya muziki uwe kwenye thamani na mambo mengine mengi,” amesema Lamar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents