Burudani

Linah akiri kuwa na mtihani wa kufanya wimbo utakaozidi hadhi ya ‘Ole Themba’

Baada ya kufanya wimbo mkubwa zaidi katika career yake, ‘Ole Themba’, Linah amedai kuwa mtihani alionao sasa ni kufanya wimbo mpya wenye kiwango cha aina hiyo au zaidi ili kuepuka kurudi hatua nyingi nyuma.

Linah Sanga

Linah amesema hataki kutoa wimbo ulio chini ya kiwango.

“Mashabiki wangu waendelee kukaa tayari kwa sababu project ya Ole Themba ilikuja kimya kimya na hii pia namshukuru Mungu itakuja kimya kimya,” ameiambia Bongo5. “Kwahiyo wategemee kitu kikubwa zaidi ya Ole Themba kutoka kwangu kwa sababu siku zote unavyofanya kitu cha kwanza kikubwa kinachofuata inabidi utengeneze kitu kikubwa zaidi. Kwahiyo namshukuru Mungu kuna vitu vingi katika project zangu. Kuna kolabo na video nyingine. Wimbo utatoka ndani ya mwaka huu inshallah mwezi ya kumi na mbili.”

“Mpaka sasa hivi bado sijajua kama itakuja na video au audio pekee, kwa sababu kuna vitu vingi bado sijakaa na menejimenti yangu tukakubaliana. Audio tayari nimeshafanya nategemea kufanya video hivi karibuni. Hata ikitangulia audio, video itakuwa iko tayari, nafanya video kubwa siwezi kusema sasa hivi.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents