Burudani

Lil Wayne na Christina Milian wadaiwa kuwa wapenzi!!

Lil Wayne ana watoto wanne ambao kila mmoja ana mama yake na sasa huenda akaongeza orodha ya ‘mababy mama’ iwapo uhusiano wake na Christian Milian ukiwa kweli.

article-0-1FB469C400000578-894_634x480

Mwezi mmoja baada ya kuachana na mpenzi wake Jas Prince, Christina Milian anadaiwa kuanzisha uhusiano na bosi wake wa Young Money Lil Wayne. Wawili hao walipigwa picha wakitembea wakiwa wameshikana mikono kwenye hafla ya ESPYS jijini Los Angeles, Jumatano hii.

Na sasa vyanzo vimeuambia mtandao wa Us Weekly: ‘It’s totally true. They are hooking up.’

article-2675365-1F460E5F00000578-710_634x825

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Christina, 32, na Lil Wayne, 31, kuwa pamoja kwakuwa mwishoni mwa June walionekana tena kwenye BET Awards afterparty. Hata hivyo mtandao wa TMZ, umedai kuwa tetesi za kuwa mastaa hao ni wapenzi si za kweli na kwamba wanatafuta tu kiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents