Burudani

Lil Wayne kwa Birdman: Tha Carter V haitoki hadi unilipe mkwanja wangu

Birdman alikuwa akijidanganya tu pale alipodai kuwa album ya Lil Wayne, Tha Carter V inatoka hivi karibuni, kwa mujibu Lil Wayne mwenyewe.

Vyanzo vilivyo karibu na Weezy, vimeiambia tovuti ya TMZ kuwa rapper huyo anadhani Birdman inabidi aache kujipa uhusika kwenye album hiyo inayosubiriwa kwa hamu, na kuanza kuilipia sababu hadi sasa hakuna hatua iliyopigwa katika kesi yao ya madai. Wamedai kuwa Wayne amemsikia Birdman akidai kuwa anaiweka bifu yao pembeni, lakini anaamini kuwa bosi huyo wa Cash Money anajaribu tu kuonekana mzuri mbele ya watu.

Weezy haoni dalili za kulipwa dola milioni 51 anazodai na kwamba kama hazitolipwa, hakuna linaloweza kubadilika. Pia ni Wayne ndiye mwenye master ya album hiyo. Inadaiwa kuwa wiki iliyopita Birdman alikutana na Universal Music Group kujaribu kuangalia namna ya kumlipa Wayne ili kumfurahisha.

Ni katika mkesha wa mwaka, Weezy alimchana Birdman kwa kuwaambia mashabiki, “If you see Stunna, tell him I said, ‘F*** him!'”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents