Burudani

Lil Wayne kuondoka Cash Money pamoja na Drake na Nicki Minaj

Nicki Minaj na Drake ni kama watoto wa Lil Wayne hivyo akiondoka Cash Money Records ataondoka nao hata kama Birdman akiwa na mipango mingine, kwa mujibu wa TMZ.

00135

Vyanzo vilivyo karibu na Lil Wayne vimeuambia mtandao huo kuwa pamoja na kutaka alipwe dola milioni nane na Birdman, Wayne anapanga kuhakikisha kuwa wasanii wa Young Money Entertainment wanabaki kuwa chini yake.

Drake, Nicki, Christina Milian, na Lil Twist wote wamesainishwa kwenye label ya Wayne. Mack Maine pia ni msanii wa YME na rais wa label hiyo.

Pamoja na kwamba Birdman ana umuhimu kwenye mafanikio ya Drake na Nicki, Weezy anaamini kuwa mastaa hao wanapaswa kwenda naye kwasababu mikataba yao ni ya YME.

Kufanya issue hiyo kuwa ngumu zaidi ni kuwa Cash Money ina mkataba wa usambazaji na wasanii wa Young Money. Hiyo inamaanisha kuwa suala hilo itabidi limalizike mahakamani japo vyanzo vimedai kuwa Lil Wayne hawezi kuondoka bila wasanii wake.

Kwenye ngoma yake ‘CoCo’, Weezy anarap: “I ain’t trippin’, I got Barbie … I got Drake too.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents