Burudani

Lil Wayne kuigawa album mpya ya ‘Tha Carter V’ katika part 1 & 2, pia aachia single mpya ‘Gotti’

Rapper wa Young Money, Lil Wayne amesema ameamua kuigawa album yake mpya ya ‘Tha Carter V’ katika sehemu mbili, album ambayo imesogezwa mbele tarehe ya kutoka.

Lil Wayne

Wizzy amesema ameamua kuifanya album hiyo iwe na sehemu ya kwanza na ya pili kwasababu ana nyimbo nyingi sana alizorekodi, kiasi ambacho angeamua kutoa mara moja angeishia kutoa album yenye nyimbo 12 au 13 tu.

“I recorded so many songs. I got too many songs. I worked way too much to give y’all half of it,” alisema.“If I would’ve dropped the album today, it would have to be 12 or 13 songs. I refuse to cheat my fans. I refuse to cheat myself.”

Baada ya tarehe iliyokuwa imepangwa mwanzo kusogezwa mbele, sasa sehemu ya kwanza ya ‘Tha Carter V’ imepangwa kutoka December 9.

Lil Wayne pia ameachia single mpya ‘Gotti’ kutoka kwenye sehemu ya kwanza ya album hiyo.

Sikiliza wimbo wake mpya ‘Gotti’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents