Burudani

Lil Wayne atishia kuishtaki Cash Money endapo itashindwa kutoa album yake ‘Tha Carter V’

Ule ugomvi wa Lil Wayne na label ya Cash Money bado unaendelea na inavyoonekana unaelekea pabaya zaidi. Inadaiwa kuwa rapper huyo sasa ana mpango wa kuishtaki label hiyo endapo itaendelea kukataa kutoa album yake ya “Tha Carter V”.

lil wayne

Vyanzo vya karibu vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Weezy ametoa ombi la mwisho kwa maandishi kwa lebel hiyo kuitoa album yake, na endapo watashindwa ataishtaki kampuni ili aweze kujiondoa kwenye mkataba nao.

Hii imekuja baada ya hivi karibuni Lil Wayne kutishia kujitoa kwenye label hiyo kwa madai ya kwa kuchelewesha kutoa album yake, malalamiko ambayo baadae yalikuja kujibiwa na Birdman kuwa album itatolewa lakini kuna mambo ya kiutawala ambayo Weezy hayajui na ni lazima yakamilishwe kwanza, na hiyo ndio sababu ya kuchelewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents