Burudani

Lil Wayne apigwa chini kama msemaji wa Mountain Dew, sababu ni kama za Rick Ross na Reebok

Baada ya Rick Ross kupigwa chini na Reebook, sasa ni zamu ya Tunechi. Lil’ Wayne amepoteza mchongo wake kama msemaji wa kinywaji cha Mountain Dew kufuatia mashairi kwenye wimbo wake Karate Chop.

lilwayne_emmett_till

Lil’ Wayne ambaye amekuwa akitumiwa kwenye matangazo ya Mountain Dew tangu mwaka 2012, ameikasirisha familia ya Emmitt Till kwenye wimbo “Karate Chop” ambapo Weezy anasikika akisema, “Pop a lot of pain pills, ’bout to put rims on my skateboard wheels … beat that p***y up like Emmett Till.”

Emmett Louis Till alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyeuawa huko Mississippi mwaka 1955 akiwa na miaka 14 baada ya kumtongoza msichana wa kizungu.

Licha ya kutuma barua ya kuomba radhi kwenye familia hiyo, ilikataliwa na ndugu zake pamoja umma kumkosoa vikali Lil Wayne.

Japo kampuni ya Pepsi haijatoa maelezo zaidi, hatua hiyo ilitangazwa na msemaji wa Lil Wayne Sarah Cunningham, aliyesema kuwa ni kutokana na kupishana kiubunifu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents