Burudani

Lil Wayne apanga kumpeleka Birdman mahakamani

Lil Wayne na Birdman wapo vitani rasmi.

weezy-birdman

Wayne anadaiwa kuwa na mpango wa kumpeleka bosi wake mahakamani baada ya njia za kawaida kumaliza tofauti zao kushindikana. Mtandao wa TMZ umedai kuwa wawili hao walijaribu kuyamaliza kifamilia zaidi lakini sasa Weezy amedhamiria kumshtaki Birdman ili atoke kwenye uongozi wa Cash Money Records.

Wayne anasema Birdman amekiuka mkataba wao kwa kuhodhi album ya Tha Carter V na amesema anamdai Birdman dola milioni nane kama advance ya album hiyo.

Birdman anashikilia msimamo wake kuwa ataitoa album hiyo katika muda anaotaka yeye na sio vile anavyotaka Weezy. Rapper huyo wa Young Money ataendelea kurekodi na kuachia nyimbo zake nje ya Cash Money.

Kwenye wimbo ‘Coco’ uliopo kwenye mixtape yake mpya, Sorry 4 the Wait 2, Weezy amewachana Cash Money.

“I’m a one-man army / And if them n**as comin’ for me, I’m goin’ out like Tony / Now I don’t want no problems, I just want my money. All I got is Young Money, no more Cash, ni**a,” anarap.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents