Burudani

Lil Wayne aishtaki Cash Money, anataka alipwe dola milioni 51

Hatimaye Lil Wayne ameishtaki Cash Money akimtaka jaji avunje mkataba na label hiyo ya Birdman.

lil-wayne-birdman

Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Cash Money ilikiuka makubaliano kwenye mkataba wao kwa kushikilia mamilioni ya dola anayoidai label hiyo kwa kuchelewesha album, Tha Carter V.

Wayne anadai kuwa kwasababu Cash Money wamegoma kumlipa, ana uhuru wa kuondoka. Pamoja na kutaka kuwa huru, Weezy pia anataka alipwe dola milioni 51, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ.

Lil Wayne pia anamtaka jaji aamuru kuwa yeye ndiye mmiliki wa wasanii a Young Money wakiwemo Drake na Nicki Minaj.

Hata hivyo mtandao huo umedai kuwa kama Cash Money ikimlipa dola milioni 10 za album hiyo, Wayne hatokuwa na nafasi tena kisheria kuvunja mkataba wake.

TMZ imedai kuwa Universal, label ambayo ni wasambazaji wa Cash Money records inaweza kuingilia kati kulipa kiasi hicho na tayari inamtaka Birdman amalize suala hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents