Burudani

Lil Ommy adai mashabiki wa Afrika Kusini wanahamu na Raymond kwenye MTV MAMA 2016

Jumamosi hii ya Oktoba 22, mwaka huu zinatarajiwa kufanyika tuzo za MTV MAMA 2016 kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini lakini imedaiwa kuwa Raymond ameonekana kuvutia zaidi kwenye tuzo hizo.

ctyazkyxyaacgg2

Mtangazaji anayefanya vizuri kwa sasa kupitia Times FM na kipindi chake cha The Playlist, Omari Tambwe aka Lil Ommy ambaye ameweka kambi nchini humo kwa ajili ya kushuhudia tuzo hizo amesema kuwa mashabiki wamekuwa wakiwasubiri wasanii wengi lakini shauku yao kubwa ipo kwa Raymond wa WCB.

“Wanasubiriwa wasanii wengi lakini, shauku zaidi ipo kwa Raymond watu wengi hapa wameanza kumfuatilia, wengine wakiwa na hamu ya kumshuhudia kuzingatia ni msanii mpya halafu kipengele chenyewe kina uzito yaani msanii aliyeingia na kufanya vizuri,” Lil Ommy ameiambia Times FM.

Raymond anawani kipengele cha msanii bora anayechipukia, wao wanakiita Best Breakthrough Act akiwa na wasanii wengine kama Simi (Nigeria), Nathi (Afrika Kusini), Nasty C (Afrika Kusini), Franko (Cameroon), Falz (Nigeria) na Emtee (Afrika Kusini).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents