Promotion

Lil Ommy aanzisha Facebook TV, kuonekana kwenye kurasa za Facebook

Mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, Omary Tambwe aka Lil Ommy ameamua kuutumia mtandao wa kijamii wa Facebook kama sehemu ya chombo cha habari na kuwafikishia watu kipindi kifupi cha TV.

Lil Ommy amesema kuwa kipindi hicho ni mfano wa vipindi vinavyowekwa YouTube lakini yeye ameamua kuwahuhisha zaidi watu walioko Facebook ambao watakuwa sehemu kubwa ya maandalizi ya vipindi vya burudani.

Kwa kuanza Lil Ommy anaanza na kipindi kitakachohusisha video 5 kubwa. “Ni kipindi kitakachohusisha video tano kubwa zinazopendwa zaidi na watu. Chart itapangwa na mashabiki katika kurasa ya Facebook na kujumuishwa
kwenye ukurasa mama wa FBTV,” amesema. Amesema ndani kutakuwa na stories zinazohusu wasanii
walioingiza video hizo. “Facebook kuna fans wengi wa muziki. Nataka watu hao wawe na uwezo wa kuangalia vipindi kwa muda wao na hata kukirudia muda wowote wanaotaka.”

Kwa mujibu wa Lil Ommy, FBTV itaanza hivi karibuni. Ifuate na Like ‘FBTv’ kupitia link hii www.facebook.com/RuningaYetu . Kwa updates zaidi mfuate @LilOmmy kwenye Instagram na Twitter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents