Burudani

Lil Kim anatarajia kuwa mama, ujauzito wake umejulikana alipohudhuria ‘New York Fashion Week’

Rapper mkongwe wa Marekani Kimberly Denise Jones a.k.a Lil Kim amewasuprise watu wengi baada ya kuwasili katika New York Fashion Week akiwa na tumbo kubwa, na ndipo ilipofahamika kuwa ni mja mzito.

lil kim-4

Hip Hop Diva huyo mwenye miaka 39 ambaye ujauzito wake haukua umefahamika mpaka alipojitokeza hadharani akiwa na tumbo kubwa, alionekana kupewa uwangalizi mkubwa na walinzi wake ambao sehemu zingine ilibidi wambebe kutoka kwenye gari.

lil kim-3

Rafiki yake wa karibu Perez Hilton naye alikuja kuthibitisha juu ya ujauzito huo baada ya kupost picha yake na kuandika ‘Me and a very PREGNANT #LilKim at #TheBlonds show. Congrats, boo!!’

lil kim-1

Si huyo tu rafiki mwingine wa Kim Tamar Braxton naye alithibitisha kwa ku comment tweeter ‘Awwwww congrats @LilKim on your little one’.

lil kim-2

Hata hivyo kama alivyoficha ujauzito wake ndivyo ambavyo bado ni kitendawili cha nani ambaye yuko kwenye uhusiano na rapper huyo ambaye huenda ndiye baba wa mtoto huyo ajaye.

Mwishoni mwa mwaka jana mwezi September kulikuwa na taarifa kuwa Lil Kim alikua kwenye uhusiano wa kimapenzi na bondia Floyd Mayweather Jr.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents