Michezo

Ligi kuu Ubelgiji: Samatta apachika goli 1 kati ya matatu ya KRC Genk dhidi ya Sint-Truiden

By  | 

Nahodha wa timu a taifa ya Tanzania , Mbwana Samatta amezidi kuwasha moto katika ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama Jupiler Pro League baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata wakiwa ugenini usiku wa Ijumaa hii dhidi ya Sint-Truiden.

Mabao ya Genk yalifungwa na Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 37, Mbwana Ally Samatta dakika ya 39 na Ruslan Malinovskiy dakika ya 45.

Kwa sasa Genk wanashika nafasi ya tano katika ligi hiyo wakiwa na pointi 41 huku klabu ya Club Brugge ndio wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 52.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments