Habari

LHRC: Serikali itoe msimamo kuhusu kuondolewa kwa adhabu ya kifo

Serikali imetakiwa kutoa msimamo sahihi kuhusiana na adhabu ya kifo. Imeshindwa kufanya hivyo tangu mwaka 1994, licha ya watu kuendelea kuhukumiwa huku wadau mbalimbali yakiwemo madhehebu ya dini wakiipinga kwa madai kuwa inakiuka haki za binadamu.

bisimba

Akizungumza katika kongamano la kupinga adhabu ya kifo lililofanyika jijini Dar es Salaam,mkurugenzi wa sheria na kituo cha haki za binadamu,LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alisema, “Kwa sisi tunavyoamini kwa haki za binadamu ni adhabu inayopoteza utu wa mtu lakini ni adhabu ambayo haisaidii yule aliyefanya kosa kuweza kujirudi.”

“Lakini ni adhabu ambayo pia ikikosewa hauwezi kubadilisha. Kwahiyo kwa adhabu kama hiyo inabidi tujiangalie mara mbili kabla ya kukubali kuendana nayo,” aliongeza.

Alisema kuwa nyingi zimeshafuta adhabu hiyo zikiwemo 20 za Afrika na hivyo Tanzania haina budi kufanya hivyo pia.

Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini, viongozi wa dini na wadau mbalimbali.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents